HERI YA SIKU YA WACHAGGA, (HAPPY CHAGGA'S DAY FESTIVALS).
Ni Siku Kubwa Iliyokuwa Inaadhimishwa Kila Mwaka Siku Ya Novemba 10, Miaka Ya Kabla Ya Uhuru wa Tanganyika na Miaka Michache Baada ya Uhuru Wa Tanganyika. Siku Hii Ilisherehekewa Kitaifa Kilimanjaro Katika Ikulu Ya Mangi Mkuu wa Wachagga KDC Moshi Mjini na Katika Maeneo Mengine Ya Wamangi Kilimanjaro Nzima.
Maadhimisho Haya Yalihudhuriwa na Watu wa Rika zote Kuanzia Watoto, Wanafunzi wa Shule na Watu Mashuhuri Kutoka Ndani na Nje Ya Kilimanjaro Yalijumuisha Maonyesho Mbalimbali na Nyimbo Ukiwemo Wimbo wa Jamii/Taifa La Wachagga Kilimanjaro.
Baadhi Ya Wachagga wa Leo Wenye Angalau Kuanzia Miaka 70 na Kuendelea Bado Wana Kumbukumbu Ya Maadhimisho Haya Ambayo Yalikuwa Muhimu na Makubwa Sana Kilimanjaro.
Siku Hii Ilikuwa Maalum Kwa Ajili Ya Kuimarisha Mshikamano, Ushirikiano, Kujiamini na Kujitambua Kwa Wachagga Katika Kukuza Ustawi wa Wachagga Kuelekea Kutimiza Ndoto Kuu Ya Wachagga(Chaggas Dream).
Sisi Wachagga wa Leo, Kama Ilivyo Kwa Jamii Nyingi Zenye Kujitambua Duniani Tuna Haki na Wajibu wa Kuienzi Siku Hii Muhimu Kwetu Itakayosaidia Kuimarisha Mshikamano, Ushirikiano, Kujiamini na Kujitambua Kwa Ajili Ya Ustawi wa Jamii Yetu Ya Sasa na Vizazi Vinavyokuja.
Siku Hii Muhimu Sana Kwetu Ikarudishe Mshikamano na Upendo Baina Yetu na Kutujengea Kujiamini na Kujitambua Zaidi, Kama Jamii Makini na Inayojali Kuhusu Hatma Yake
Na Kwa Sasa siku hii itaendelea kuadhimishwa kila November chini ya Campun ya URASSA INTERTINMENT EMPIRE usipange kukosa.